Kiswahili edition of Africa Bible Commentary
John R. Stott
Kitabu hiki cha Ufafanuzi wa Biblia Katika Mazingira ya Kiafrika ni kitabu cha kipekee kuwahi kuchapishwa –maana ndicho cha ufafanuzi wa kwanza wa Biblia katika juzuu moja lililotolewa Afrika na wanatheolojia Waafrika ili kuyakidhi mahitaji ya wachungaji wa Kiafrika, wanafunzi na viongozi wa kanisa. Kwa kufasiri na kuzingatia matumizi ya Biblia katika mikutadha halisi ya utamaduni wa Kiafrika ulivyo sasa; kitabu hiki kinayaelezea Maandiko Matakatifu vizuri sana na kwa undani kwa njia bora zinazoafiki bara la Afrika kwa umuhimu wake.
Kitabu hiki cha Ufafanuzi wa Biblia Katika Mazingira ya Kiafrika kinatoa ufasiri wa sehemu kwa sehemu ambao unaambatana na muktadha wa Kiafrika unaoeleweka kwa urahisi. Isitoshe, kitabu hiki kina bei nafuu na hivyo basi kukifanya kuwa mwongozo bora sana wa kuisoma Biblia yote! Wasomaji kote duniani watafaidi na kuifurahia mitazamo mipya watakayopata hapa pamoja na jinsi mtindo wake wa moja kwa moja utakavyowahusisha kimoyo na kifikira.
SIFA KUU
Kimeandikwa na wasomi wa Biblia wa Kiafrika, katika Afrika, kwa Waafrika na ulimwengu wote.
Kina ufafanuzi unaotoa ufasiri wa Maandiko Matakatifu sehemu kwa sehemu pamoja na matumizi yake maishani
Kina zaidi ya makala nyeti 70 yanayoshughulikia masuala muhimu juu ya huduma barani Afrika sasa, na yaliyo na umuhimu kote duniani.
Kimeandikwa na waandishi 70 wa Kiafrika wanaotoka katika maeneo yanayosema Kiingereza na yanayosema Kifaransa
Kinaupiku muktadha wa Kiafrika vizuri sana kwa jinsi kinavyoyaeleza Maandiko Matakatifu pamoja na imani ya Kikristo kwa wasomaji kote duniani.
MHARIRI MKUU
Dkt. Tokunboh Adeyemo ndiye Msimamizi Mkuu wa Centre for Biblical Transformation. Hapo awali alikuwa Katibu Mkuu wa Association of Evangelicals in Africa. Ana shahada ya Uzamifu (PHD) kutoka Dallas Theological Seminary.
Download Product Info Sheet(Kielezo-Barua Ya Yakobo)